Utengenezaji wa michezo ya kuigiza ya redio nchini Tanzania Kwa mara ya pili kituo cha utangazaji cha kimataifa cha Ujerumani, Deutsche Welle (DW), kinatayarisha vipindi vya kuburudisha na kuelimisha kwa michezo ya kuigiza kwa ajili ya vijana chipukizi nchini Tanzania. Utengenezaji wa vipindi hivyo utaanza Jumatano tarehe 2 Mei hadi Juni 2, wakishiriki wachezaji wa [...]


Ufafanuzi wa kihistoria ya kidini ya kisiasa unaojenga hoja ya Wazanzibari kuukataa Muungano, miaka karibuni 50 baada ya kuundwa kwake. Angalia vidio za sehemu ya mihadhara inayotayarishwa na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu ya Zanzibar (UAMSHO).


Maoni ya wananchi katika Kongamano la Katiba lililotayarishwa na Baraza la Katiba la Zanzibar katika mfululizo wa kutoa elimu kwa Wazanzibari kuwatayarisha kwa Katiba Mpya ijayo katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Angalia sehemu ya vidio za makongamano hayo.


Jeshi la Sudan limesema linasonga mbele kuukomboa mji wa Heglig ambao umetekwa na majeshi ya Sudan ya Kusini kwa siku ya tatu sasa, huku Sudan ya Kusini imesema itaondoka tu kwenye eneo hilo lenye utajiri wa mafuta, ikiwa Umoja wa Mataifa utapeleka wanajeshi wake. Endelea kusoma habari hii. Chanzo: Deutsche Welle Kiswahili, 14 Aprili 2012


Rais Jakaya Kikwete ameiapisha Tume ya Katiba, kama inavyojuilikana, ambayo jukumu lake ni kukusanya maoni ya Watanzania juu ya katiba wanayoitaka. Katika uapishaji huo uliofanyika Ikulu ya Magogoni, Ijumaa ya 13 Aprili 2012, Rais Kikwete aliwakumbusha ’ambao’ hawautaki Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wajuwe kuwa si Tume yake aliyoiunda ya kuwasaidia kupata muradi wao.


Rais wa Malawi, Bingu wa Mutharika, amefariki dunia mjini Lilongwe, baada ya kuugua kwa muda mfupi. Mwanzoni redio ya taifa ilikuwa imetangaza kwamba Mutharika, mwenye miaka 78, angelipelekwa Afrika Kusini kwa matibbabu zaidi, lakini inaonekana kwamba alishafariki dunia wakati alipofikishwa hospitali. Kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo, Makamu wa Rais Joyce Banda, ndiye anayechukuwa [...]


“Tunatangaza rasmi uhuru wa Azawad kuanzia leo,” alisema Mussa Ag Attaher, ambaye aliongeza kwamba waasi hao wataheshimu “mipaka ya mataifa mengine.” MNLA imesema kwamba kutokana na mafanikio yao ya kuliteka eneo wanaloliita Azawad, wanasimamisha mara moja operesheni za kijeshi kuanzia usiku wa jana. Katika tangazo hilo “la uhuru”, Ag Attaher alisema: “Tunakubali dhamana na dhima [...]