Skip to content

Membe, Maalim Seif wapokewa kishujaa Unguja

Umma mkubwa wa watu walijitokeza leo (Agosti 9) kwenye mapokezi ya wagombea urais wa Zanzibar na Muungano wa chama cha ACT-Wazalendo, ambao walifika kwa mara ya kwanza kisiwani Unguja tangu wateuliwe na vyama vyao wiki iliyopita.

Maalim Seif Sharif Hamad, anayewania tena urais wa Zanzibar kwa mara ya sita mfululizo, aliambatana na Benard Membe anayewania urais wa Jamhuri ya Muungano akiwa na mgombea mwenza wake, Profesa Omar Fakih Hamad, pamoja na Kiongozi wa Chama Zitto Kabwe.

Mgombea urais wa Tanzania kwa tiketi ya ACT-Wazalendo, Benard Membe (kulia) akiwa na mgombea mwenza wake, Profesa Omar Fakih Hamad, wakiwapungia mkono maelfu ya wafuasi wao kisiwani Unguja leo.

Waliwasili kwenye Bandari ya Malindi majira ya mapema asubuhi na kukuta tayari umma umeshajaa bandarini hapo na barabara zote kuelekea Ofisi za ACT Wazalendo, Vuga, katikati ya Mji Mkongwe wa Zanzibar.

Msafara wa viongozi hao ulipita mitaa kadhaa ya Mjini Unguja ukisindikizwa na maelfu ya wafuasi wao waliokuwa wakiimba na kucheza, huku wengine wakibeba mabango yanayosomeka: “SHIKAMOO MAALIM SEIF” – kauli inayoonekana kuwa kibwagizo cha kampeni za uchaguzi wa mwaka huu.

 

Leave a Reply