Skip to content

CategoryUchambuzi/Analysis

“Kulikoni matumaini ya Zanzibar?”

Zanzibar yenyewe hivi ilivyo ni taifa lililodumaa. Haina maendeleo ya maana ambayo serikali inaweza kujivunia. Ilishangaza hivi karibuni kumsikia Rais wa Zanzibar , Dkt. Ali Mohamed Shein, akilalamika kwamba Zanzibar ikilingalishwa na jiji la Dar es Salaam iko nyuma sana hasa kwa miundombinu.

Makubaliano ya Serikali na Barrick Gold Changa la Macho

Licha ya makubaliano haya ya hovyo na yasiyo na tija, Serikali yetu imetoa ‘waiver’ (msamaha) kwa Barrick kutoorodhesha hisa kwenye Soko la Hisa la Tanzania. Sheria ya Madini ya mwaka 2010 (Wakati wa Waziri William Ngeleja) na Kanuni zake iliweka sharti kwamba ni lazima makampuni ya madini yauze 30% ya hisa kwa Watanzania kwenye soko la Hisa la Tanzania.

SUDAN: Nyufa ndani ya jeshi; nyufa ndani ya upinzani

Ukweli wa mambo ni kwamba al Bashir alipoangushwa Aprili mwaka huu, aliyeangushwa alikuwa ni yeye binafsi lakini si utawala wake. Na huo utawala wake, au mabaki ya utawala wake, ndio unaomkinga hivi sasa. Unamkinga yeye na, wakati huohuo, unajikinga wenyewe. Ndio maana wenye kuuongoza wanafanya ukaidi kuondoka madarakani moja kwa moja.