Kwa dhati kabisa, simuoni mgombea wa akina Polepole kuwa na uwezo wa kukabili changamoto hizo. Ndio maana inabidi kurudi kwa Polepole kumuomba awajibu Wazanzibari masuala ya msingi. Maana yeye anayejinadi kuwa ataleta maendeleo ndiye kikwazo cha mwanzo cha mgombea wao.
Maalim Seif, ambaye kama akipitishwa atakuwa anawania nafasi hiyo kwa mara ya sita mfululizo, alisema kuchukuwa kwake fomu hiyo hakumaanishi kwamba milango imefungwa kwa wanachama wengine wenye nia ya kuwania wadhifa huo.
Wafuasi na wanachama kadhaa waliojitokeza kwenye ukumbi wa ofisi za ACT Wazalendo Micheweni waliimba kwa furaha na hamasa wakimuhakikishia kiongozi wao huyo kwamba bado wana imani naye kuwania nafasi ya urais wa Zanzibar.