Habari
SMZ ACHENI KUISHUTUMU MAREKANI JIREKEBISHENI
MAREKANI imewatahadharia raia wake kutopanga safari zisizo za lazima kwenda Pemba, baada ya kutokuwa na imani ya usalama katika eneo hilo wakati huu wa kuekea uchaguzi mkuu wa mwakani. Pamoja na tahadhari hiyo, raia wa Marekani wanaofika nchini kwa ajili ya kwenda Zanzibar hutakiwa kufika kwanza katika ubalozi wa nchi hiyo uliopo Dar es Salaam ili kuhakikisha usalama wao wawapo nchini. Endelea kusoma tahriri ya gazeti la Mwananchi
MAREKANI YAONYA RAIA WAKE KUTOENDA ZANZIBAR
MAREKANI imetahadharisha raia wake kuepuka safari zote zisizo za lazima visiwani Zanzibar kutokana na hofu ya kuibuka kwa zinazohusiana na uchaguzi wakati visiwa hivyo vikiwa kwenye zoezi la kuandikisha wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwakani. Tahadhari hiyo, ambayo inaweza kuathiri kwa kiasi kikubwa uchumi wa visiwa hivyo unaotegemea utalii, imetolewa wakati Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) ikiwa imesimamisha zoezi hilo la kuandikisha wananchi kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura baada ya kutokea vurugu zilizosababisha watu kadhaa kujeruhiwa kisiwani Pemba. Endelea kusoma habari hii
RACE, REVOLUTION AND THE STRUGGLE FOR HUMAN RIGHTS IN ZANZIBAR (PART 8)
In the 1930s(and even now), however, Zanzibar Town was divided into two main areas, Stone Town and Ng’ambo.The well-to-do people lived in Stone Town, and the less well-offlived in Ng’ambo. Ng’ambo started as a poor man’s land on the other side of the creek from Stone Town.That is what Ng’ambomeans in Swahili,“the other side. ”Stone Town had stone buildings three and four stories high, but Ng’ambo mostly had ground-level buildings constructed of mud, cement, and thatch.The more prosperous had roofs made of corrugated iron. Mostly Arabs and Indians lived in Stone Town; very few Africans lived on that side of the creek; they would come for work in the day and return to Ng’ambo in the evenings. Ng’ambo was more ethnically mixed than Stone Town. There were Arabs and Comorians living near the creek, but the further you went into the interior,the more Africans you encountered. Read more
That the United States’ President Barack Obama is a brilliant man is indisputable. Whether that brilliance is attributable to accidental inter-racial mating of two gifted parents may not be so clear. What is certain is that Obama comes from an American society that earlier in the 20th century still believed in ‘eugenics,’ purposeful selective breeding process to produce quality offspring. Read more of this Ali Mazrui’s article
MUSLIM CLERICS UNVEIL OWN MANIFESTO OF 2010 ELECTION
The Political Committee of the Council of Muslim Clerics yesterday launched a 45-page guideline for Muslims for the 2010 General Elections. The guideline, entitled ‘Shura ya Maimamu Tanzania Kamati Kuu ya Siasa, Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2010’ “Muongozo Kwa Waislamu”, touches on a wide range of social and political issues in the country. Hundreds of people, among them representatives of 22 Mainland regions as well as Zanzibar and Pemba, attended the launch in Dar es Salaam. Read more
JUMBA LA KULELEA WATOTO FORODHANI KUGEUZWA MAKUMBUSHO
JUMBA lililokuwa la kulelea watoto yatima Forodhani linatarajiwa kugeuzwa makumbusho ya usafiri wa baharini ili kutowa fursa kwa wageni na wenyeji kupata historia ya mambo hayo hapa Zanzibar. Jumba hilo, ambalo awali yake walikuwa wakiishi watoto yatima waliokuwa na uangalizi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambao kwa sasa wamehamia katika jengo jipya lililojengwa na Mke wa Rais wa Zanzibar ambae pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya ZAYEDESA, Mama Shadya Karume, huko Mazizini mjini hapa. Endelea kusoma habari hii
MIFUKO YA PLASTIKI BADO INATUMIWA KINYEMELA ZANZIBAR
BAADHI ya wafanyabiashara wa Zanzibar wameonekana kuendelea kuuza mifuko ya plastiki na kuupuza amri ya Serikali licha ya kupiga marufuku matumizi ya mifuko hiyo hapa nchini. Hali hiyo imebainika kufuatia mwandishi wa habari hizi kutembelea katika maeneo tofauti ya biashara katika Manispaa ya mji wa Zanzibar na vitongoji vyake nakubaini kwamba katika maeneo mengi ya biashara bado inaendelea kutumika. Wafanyabaishara wadogo wadogo wanaoza bidhaa katika maeneo mbali mbali maarufu ya biashara mjini hapa wamekuwa wakiwatilia bidhaa wateja wao licha kwamba wamekuwa wakiificha mifuko hiyo. Endelea kusoma habari hii
BODI YABAINI MAZIWA YASIYOFAA KUWEPO ZANZIBAR
BODI ya Udhibiti wa Dawa, Vyakula na Vipodozi Zanzibar imefanya msako wa kushitukiza katika maduka mbali mbali kutafuta maziwa aina ya S26 yanayosadikiwa hayafai kwa matumizi ya binadamu. Bodi hiyo katika msako huo pia imefanikiwa kukamata kiwango kidogo cha maziwa na imeyapiga marufuku kuuzwa na kutumiwa na wananchi Zanzibar. Msako huo ulifanyika jana katika maduka tofautio mjini hapa baada ya kubainika kuwapo maziwa hayo yenye namba moja chini ya jina lake yanayoaminika kuwa na athari kwa wanaoyatumia; hasa watoto. Endelea kusoma habari hii
ZANZIBAR WITHDRAWS PASSPORTS OF UNREGISTERED COMORIANS
Zanzibar authorities have embarked on a special exercise to withdraw passports issued to Zanzibar residents originating from Comoro who had failed to apply for citizenship as directed in 1968 by the first President of the Isles, the late Sheikh Abeid Amani Karume. Read the story
JUST WHO IS TO BLAME OVER THE Z’BAR PVR MESS?
The exercise of registering voters in the Permanent Voter Registrar (PVR) in Pemba has been brought to a standstill for more than two weeks now. It could be too early to say when it would resume as the situation is still at shaky. However, there is one fact on the drawing board: in spite of its necessity to the democratization process, the exercise that prohibits a good number of citizens from participating in their civil and democratic rights can not be called democratic. Read more
ZANZIBAR ISP CONNECTED TO SEACOM
A Zanzibar-based Internet Services Provider (ISP) has become the latest Tanzanian company to connect with Seacom submarine fibre optic cable. Zanlink whose trade name is Zee Communications Limited becomes the first ISP in the country to be connected with the cable. This is expected to increase competition among ISPs, improve service delivery and lower prices. The Tanzania Telecommunications Company Limited and SimbaNet are linked up with Seacom. Read more
TUNAINASUAJE ZANZIBAR KATIKA MGANDO HUU?
SUALA uandikishaji wapiga kura hapa Zanzibar sasa linaanza kuchukua sura nyengine pale wiki iliyopita Serikali ya Zanzibar ilipojuburi tamko lililotolewa na Umoja wa Ulaya, Marekani na Japan lililosema na kutoa wito kuwa Serikali zinapaswa kuhakikisha kuwa Watanzania wote wanapata haki ya kujiandikisha katika daftari la wapigakura na kwamba SMZ iondoshe kasoro zilizojitokeza katika zoezi hilo. Endelea kusoma
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imetangaza rasmi kutumia nguvu za dola kupambana na makundi ya watu wanaojihusisha na vitendo vya kigaidi katika Kisiwa cha Pemba. Msimamo huo ulitolewa jana na Waziri wa Nchi Afisi ya Waziri Kiongozi, Hamza Hassan Juma katika Ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam wakati wa kongamano la siku moja, lililoandaliwa na Chama cha Wananchi (CUF) kwa lengo la kujadili hali ya kisiasa kisiwani Zanzibar. Endelea kusoma
ZANZIBAR’S ACADEMICIANS FORM NGO
ZANZIBAR’s academicians living abroad and home have formed a research NGO dubbed ‘Zanzibar Institute for Research and Public Policy (ZIRPP), that will function as a think-tank, research and policy based institute. Addressing a gathering during the launching ceremony, the acting chairman of the Board of Trustees of ZIRPP, Mr Muhammad Yussuf, said that the institute “will mobilize un-tapped human resources of Zanzibaris from within Zanzibar and in the Diaspora.” Read more
KIKWETE, KUPI NDIKO KUCHEZEA MAPINDUZI YA ZANZIBAR?
“Nina wasi wasi mkubwa na kauli hii ya Kikwete kuendeleza wazo moja (cliché) kuwa Mapinduzi hayachezewi, yasichezewe na hayachezeleki wakati anajua Visiwa hivi kama ilivyo Tanzania vimo katika siasa za ushindani wa vyama. Inawezekana kabisa, ingawa yeye anasema kuna nafasi ndogo kwa chama cha CUF kuweza kushinda uchaguzi kama si wa 2010 basi mwengine wowote unaofuata, na kwa kauli ya Kikwete kuendeleza dhana hiyo kongwe ya “Mapinduzi hayachezewi” ina maana kuwa CUF haitapewa Serikali.” Soma makala hii ya Ally Saleh…
UCHAGUZI MDOGO MAGOGONI MEI 23
“Katika kikao chake kilichofanyika jana tarehe 29 2009 tume ya uchaguzi Zanzibar iliitiitafakari kwa kina taarifa hiyo ya spika na masharti ya uchaguzi, 1984 kifungu 45 (b), nachukua nafasi kukikinukuu hicho, endapo uchaguzi mdogo umepangwa kufnayika siku ya uteuzi itakuwa si chini ya miezi minne na si zaidi ya miezi 25 baada ya tukio lililopelekea kufanyika kwa huo uchaguzi mdogo…” Soma habari hii…
WAZIRI KIONGOZI ATAKA KUFAGIA BARABARA
“Nahodha amelazimika kuchukua uamuzi huyo kutokana na kubaini wafanyakazi wa baraza la mji wamekuwa dhaifu katika kutekeleza majukumu yao ya kufanya usafi katika maeneo mbali mbali ya mji pamoja na barabara za mjini kuwa chafu mno.” Soma habari hii…
ZANZIBAR YAJIUZA VYEMA
Serikali ya Mapindizi Zanzibar inasema Zanzibar imenufaika sana katika kujitangaza kwa wawekezaji katika sekta ya utalii na ushirikiano kwa nchi na mashirika mbali mbali ya misaada ya kimataifa duniani. Soma habari hii…
MAFUTA NI MALI YA WAZANZIBARI –SMZ
“Hao wanaosema hakuna mie nasema hakuna teknolojia ya 100% ,lakini ninachoweza kusema ni kuwa uwezekano wa kuwepo mafuta Zanzibar upo na hilo tutalijua zaidi tukianza kuchimba. Sasa ikiwa tutapata kinibu, geloni au pipa, hayo yatakuwa ni maumuzi ya Wazanzibari. Kama mafuta kidogo tutajipaka na kama gesi kidogo basi tutanusa. Kule Tundauwa Pemba mafuta yanakuja yenyewe. ” Soma habari hii…
SMZ IMESHINDWA KUTIMIZA AHADI
“Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imekiri kushindwa kutimiza ahadi zake zilizotoa katika kikao cha Baraza la Wawakilishi kuwa wananchi hawatalipa maji hadi hapo maji yatakapoweza kutoka bila ya kusita kwa muda wa masaa 24.” Soma habari hii…
BARAZA LA BIASHARA LA ZANZIBAR KUONDOA KERO ZA MUUNGANO?
Kuzinduliwa kwa Baraza la Biashara la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni moja ya hatua muhimu ya mabadiliko ya sekta ya biashara nchini. Hayo wameelezwa wajumbe wa baraza la wawakilishi na Waziri wa Nchi Afisi ya Waziri Kiongozi, Hamza Hassan Juma wakati akitoa ufafanuzi wa utatuzi wa kero za muungano katika Baraza la Wawakilishi mjini hapa. Soma habari hii…
SMZ YAKANUSHA UPENDELEO KATIKA TENDA YA USAJILI WA MAGARI
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema haina ubaguzi wowote katika upasishaji wa tenda za serikali zinazotolewa kwa wafanyabiashara na kinachoangaliwa na vigezo na sifa pekee. Soma habari hii…
MSWADA WA MAMLAKA YA BAHARI WAPITA KWA TABU BARAZANI
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi jana wamepitisha Mswada wa Sheria ya Kuanzisha Mamlaka ya Kusimamia Usafiri Baharini na Mambo Yanayohusiana na hayo huku baadhi ya wajumbe wakikataa kuupitisha kutokana na kasoro nyingi kuwemo katika mswaada huo. Soma habari hii…
FIGO NA MOYO YAWAPELEKA WAZANZIBARI NJE KWA WINGI
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ya Zanzibar imesema kuwa wagojwa waliopelekwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu kwa mwaka 2007 ni wagonjwa 90 ambao wameigharimu serikali shilingi 214, 500,000. Soma habari hii…
UHURU WA DISEMBA 10 NA KUTIBU VIDONDA VYA HISTORIA
“Mkurugenzi huyo alisema maandishi ya baadhi ya shahada yameanza kupotea na kusomeka kwa taabu na kwamba hali hiyo inaweza kuwa mbaya zaidi, baada ya miaka mitatu kwani picha alama ya dole gumba na saini zimeanza kupoteza hadhi yake.” Endelea kusoma habari hii…
“Mjadala mkubwa umefanywa iwapo vyama vilivyokabidhiwa uhuru Zanzibar Nationalist Party ZNP na washirika wake Zanzibar and Pemba People’s Party ZPPP vilistahiki heshima hiyo kwa maelezo kuwa Afro Shirazi ndio iliokuwa ikidhulumiwa kwa mipango ya Ufalme na Mwingereza. Tuseme tukubali hivyo kuwa ASP ilikuwa na uungwaji mkono mkubwa zaidi na kuwa ilikuwa ikishinda chaguzi zote ambazo zilifanyika Zanzibar na ndio yenyewe ilistahiki pale Disemba 10, 1964, jee ni sahihi kuwa kulirekebisha hilo kulistahiki kufanywa Mapinduzi?” Endelea kusoma makala hii ya Ally Saleh…
MWAKILISHI WA MAGOGONI AFARIKI
“Daud alifariki usiku wa kuamkia jana jijini Dar es Salaam, wakati akiwa njiani kupelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kutoka hoteli ya Crown ya Kariakoo alikokuwa amefikia baada ya kuzidiwa. Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Kiongozi, Hamza Hassan Juma zinaeleza kuwa saa 7:00 usiku juzi mwakilishi huyo alizidiwa akiwa chumba namba 105 katika hoteli hiyo, mkewe aliwaamsha baadhi ya wapangaji wa hoteli ili kumkimbiza MNH lakini alifia njiani.” Endelea kusoma habari hii…
BANDARI MPYA IWE FURSA YA KUKUZA UCHUMI WA ZANZIBAR
Kwa wengi wasiojua bandari ya Zanzibar ilikuwa na umuhimu mkubwa katika eneo hili la Bahari ya Hindi kwa kuwa ilikuwa ni kituo kikubwa cha kutia nanga meli zilizokuwa zikitoka chini ya Afrika kutokea Marekani na juu ya Afrika kutoka Asia na hata Ulaya. Zanzibar ilikuwa ikitawala ukanda wa pwani ya Afrika Mashariki kutoka chini ya Somalia mpaka Sofala, Mozambique, ilihitaji bandari yenye uwezo na haiba. Mwaka 1892 ilitangazwa nia ya kuifanya Zanzibar Bandari Huru wazo ambalo halikuwahi kutimizwa kikamilifu na hata baada ya nia hiyo kusisitizwa upya katika miaka ya hivi karibuni basi bado imekuwa ni ndoto. Soma makala hii…
SUZA TO GRADUATE ITS 4TH INTAKE
- The State University of Zanzibar (SUZA) wishes to announce the names of prospective graduands for
the 4th Graduation Ceremony to be held on Saturday 29th November, 2008 at 03.00 p.m at Victoria Garden, Mnazi Mmoja.
- The Chancellor of the State University of Zanzibar and the President of Zanzibar, His Excellency Dr. Amani Abeid Karume will confer the University awards.
- Graduands are requested to attend the rehearsal on Thursday 27th November, 2008 starting at 8.00 a.m. Those who will fail to attend the rehearsal will be awarded their awards in absentia.
- For the occasion, every graduand will have to rent a graduation robe by paying non-refundable Tshs. 10,000/-. Robes will be available from Monday 24th November, 2008 at the SUZA Procurement Office, Vuga Campus.
- Graduands are required to make their own travel and accommodation arrangements and the State University of Zanzibar is not liable to reimburse any expenses. For more information about SUZA, please visit http://www.suza.ac.tz/
WAZANZIBARI KUKUTANA LONDON KUZUNGUMZIA KHATMA YA NCHI YAO
London, Uingereza
Jumuiya ya Wazanzibari waishio nje, MUWAZA, imeandaa kongomano kubwa la kimataifa kuhusu khatima Zanzibar litakalofanyika jijini Londono, Uingereza. Kongamano hilo la aina yake litahudhuriwa na maelfu ya Wazanzibari na wahadhiri kutoka vikuu na viongozi mashuhuri kutoka ndani na nje ya Tanzania watazungumzia kuhusu Muungano wa Zanzibar na Tanganyika, Haki za Kisheria za Raia wa Zanzibar, na Jinsi ya Kuleta Maendeleo kwa Wananchi na nchi ya Zanzibar.
Wazanzibari kutoka pembe zote za dunia wanaalikwa katika mkusanyiko huu wa aina yake unaotoa fursa ya kuipatia fursa Zanzibar. MUWAZA ni jumuiya iliyoundwa na Wazanzibari wanaoishi katika nchi za Ulaya kwa lengo la kuwakusanya pamoja Wazanzibari wote kuiletea maendeleo Zanzibar.
SMZ YAKIRI MIGOGORO YA KISIASA KIKWAZO
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imekiri kuwa migogoro ya kisiasa Zanzibar imekuwa chanzo cha kuchelewesha utekelezaji wa mipango ya maendeleo kwa wananchi wake. Tamko hilo lilitolewa juzi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Kiongozi, Hamza Hassan Juma, alipokuwa akifungua mafunzo kwa watendaji wakuu wa wilaya wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kutoka wilaya 10 za Zanzibar. Soma habari hii…
RAIS WA ZANZIBAR AWE MAKAMO WA RAIS
SUALA la kero za Muungano ambalo limekuwa likilitikisa Bunge mara kwa mara katika siku za hivi karibuni na wakati mwingine kuzua mjadala mzito ndani na nje ya Bunge, jana limeibuka tena baada ya Mbunge wa Viti Maalumu, Riziki Juma (CUF), kuhoji sababu za kuondolewa kwa Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais wa Serikali ya Muungano. Soma habari hii…
BADEA YAIKOPESHA MABILIONI ZANZIBAR
BENKI ya Kiarabu ya Maendeleo na Uchumi ya Afrika (BADEA) imetoa mkopo wa sh bilioni 6 kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), ili kufanikisha ujenzi wa shule za sekondari mbili za Unguja na Pemba. Soma habari hii…
WAWAKILISHI WALALAMIKIA MAFISADI KUFUMBIWA MACHO
BAADHI ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, wamesema vitendo vya ubadhirifu wa mali za umma vimekuwa vikifanyika katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) bila ya wahusika kufunguliwa mashitaka. Soma habari hii…
ZANZIBARIS ARE ALSO OWNERS OF BoT
Relevant documents from the defunct East African Currency Board seen by The EastAfrican at the time show that Zanzibar is a legitimate shareholder in the Bank of Tanzania. Documents show that Zanzibar, Tanganyika and the United Republic contributed BoT’s initial capital. Read more…
This decision follows a formal communications from the International Food Safety Authorities Network of the World Health Organisation that Chinese children who consumed infant formula manufactured from milk contaminated with melamine were suffering kidney damage. Read more…
Mfanyabiashara maarufu wa mjini Zanzibar, Nassor Abdallah Khalfan, 50, amekutwa ameuawa kikatili nyumbani kwake, baada ya watu wasiojulikana kumchoma kwa visu na kumuacha amekufa kwenye nyumba yake iliyo Mtaa wa Kikwajuni. Soma habari kamili…
ZANZIBAR PRESIDENT LAUDS IRAN’S ACHIEVEMENTS
Zanzibar’s President Amani Karume here on Saturday lauded Iran’s great achievements in different areas in the past three decades. Read more…
Baada ya watu wasiojuilikana kujitokeza juzi mjini Zanzibar na kutawanya vikaratasi vinavyomtaka Waziri wa Nchi Afisi ya Makamo wa Rais (Muungano), Mohammed Seif Khatib, kuwacha kabisa azma na harakati za kuwania uraisi wa Zanzibar hapo 2010 kwa kuwa haitetei Zanzibar, sasa Waziri huyo anajitetea kwamba anaonewa bure na kwamba yeye si adui wa Zanzibar. Soma habari kamili hapa.
SMZ YATAKIWA KUREKEBISHA MAGEREZA
TUME ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora Tanzania imeitaka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kurekebisha hali ya magereza yake ambayo yameonekana kuwa na msongamano mkubwa huku yakichanganya watoto na watu wazima. Endelea kusoma habari hii.
ABIRIA WAKWAMA KWENDA ZANZIBAR
ZAIDI ya abiria 300 waliokata tiketi za kwenda Zanzibar kwa kutumia boti iendayo kwa kasi ya Ms Sepideh juzi walilazimika kurudishiwa fedha zo baada ya wafanyakazi wa boti hiyo kugoma kuondoka wakishinikiza kulipwa mishahara yao ya mwezi wa Oktoba na fedha ya chakula. Endelea kusoma habari hii.
Zanzibar is among four countries in Africa that have reduced the burden of malaria by 50 percent or more between 2000-2007, according to the World Malaria Report 2008. Read more.
CUF NA CCM LUGHA MOJA UMOJA WA WAZANZIBARI
Baada ya kusoma habari hii, Profesa Ibrahim Noor Sharif alisema hivi: “Sijapatapo kusikia, tokea Januari 1964, khabari za Zanzibar zilizonifurahisha kama hizi alizoziandika Bi Salma Said. Shukrani zote ni zake yeye Mwenye-enzi Mungu Subhanahu wa Taala. Namuomba Mola wetu kwa dhati hayo waliyoyatamka Wahishimiwa Al-Hujjaj Amani Karume, Maalim Seif na Imamu Mkuu wa Masjid Jibril, Sheikh Abrahman Habshi yafuatiliwa na vitendo. Namuomba Mola Karimu Rahimu ayataqabalie matakwa hayo na iwe ndiyo mwisho wa kusokotana kisiasa na mwisho wa Wazanzibari kusononeka na kila hali mbaya waliyonayo. Naomba wanasiasa na wananchi wazifuate naswaha njema kwa vitendo vyema vinavyotokana na dhati ya nafsi zao; vitendo ambavyo Mwenye-enzi Mungu Subhanahu wa Taala kwa Rehma zake inshaAllah atazitilia baraka. AlLahumma Amin.” Soma habari yenyewe
MOHAMMED SEIF HATAKIWI ZANZIBAR?
“Watu wasiojulikana wamesambaza vikaratasi katika Manispaaa ya Mji wa Zanzibar vinavyomtaka Waziri wa Nchi Afisi ya Makamo wa Rais (Muungano), Mohammed Seif Khatib, kutojiingiza kabisa katika nafasi za kugombea Urais wa Zanzibar katika uchaguzi Mkuu ujao wa 2010. Vikaratasi hivyo ambavyo vimesambazwa katika sehemu mbali mbali vimemtaka Waziri Khatib kusahau ndoto za kutaka uongozi katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ikiwemo ile nafasi ya urais ambayo anatajwa kama ni miongoni mwa watu watakaojitokeza kuwania kinyang’anyiro hicho.” Endelea kusoma habari hii
TAFADHALI BONYEZA HAPA KUCHANGIA MAONI YAKO. UNASHAURIWA KUANDIKA MADA YA KILE UNACHOKICHANGIA.




