jump to navigation

Utamaduni na Fasihi

WAMEKUPIGA KWA NINI?

WAMEKUPIGA KWA NINI?

WAMEKUPIGA KWA NINI?

Mwanangu unanijia, hali unatiririka, damu muili mzima

Tumboni ninaumia, machango yanikatika, moyo wapwita; wauma

Lipi limekutokea, shenzi walolaanika, washakupiga kwa vyuma?

Kwa nini wamekupiga? Endelea kusoma shairi hili.

NENDE WAPI?

NENDE WAPI NIKAPATE HAKI YANGU?

NENDE WAPI NIKAPATE HAKI YANGU?

Niende wapi kwa nani, nikapate haki yangu?

Nani wa kunithamini, wa kujuwa utu wangu___

Ikiwa mahakamani, ndipo ninyimwapo changu

Ni wapi hapo pengine? Endelea kusoma shairi hili

HUNA TENA USHUPAVU

HUNA TENA USHUPAVU

HUNA TENA USHUPAVU

Ushavyoila ndoana, papa huna ushupavu

Hata ukawanawana, kwa vishindo na maguvu

Ndoana ishakukwama, huna tena uwerevu

Na kila tukivutana, ndipo twakuzidi nguvu

Endelea kusoma shairi hili

ZAMA MAUTI YAKIJA…

Zama za kufa zikija:

Zije ningali ni mtu, sijageuka nguruwe

Sijakuwa nyama mwitu, azaaye na wanawe

Zije bado nina utu, hiondoka nililiwe

Hishima tuwe pamoja.

Endelea kusoma shairi hili

ZANZIBAR NI NJEMA!

Juwa lenda machweoni

Linazama baharini

Dhahabu yake launi

Na mvuvi kidauni

Arudi toka mavuvi

Endelea kusoma shairi hili

HABIBI ZENJ

Ungalinipa dhahabu, almasi na yakuti

Na makasiki ya fedha, na mabakuli ya wati

Kwa kutaka niiwache, Zenji yangu siiwachi

Ni radhi utwae yote, lakini si kitu hichi

Kwamba ndiyo roho yangu!

Endelea kusoma shairi hili

KUWEZA KUTAKA

Madhali hatujataka, hatunyanyuki, tungawa wa kunyanyuka

Tungawa wa kunyanyuka, hatuinuki, tupaswapo kuinuka

Tupaswapo kuinuka, hatujishiki, sababu ya kutotaka

Zama za kuja kutaka, za kutaka jiinuwa, ‘tajiinuwa wenyewe.

Endelea kusoma shairi hili

WATAAMKA

Wataamka, nasema wataamka, nalo nelisema kale

Wataamka, punde muda ukifika, kwanza wawache walale

Wataamka, kwa majogoo kuwika, na jua kuvya mishale

Wataamka, kwa kwisha kupambazuka, na kwa kwisha tongo zile!

Endelea kusoma shairi hili

KESHO TUTAINUKA

Kuna yapi ya uchungu, kama kumwagiwa damu?

Ya watoto damu changa, ‘liyotarajiwa

Ya vijana damu mbichi, ‘liyotegemewa

Ya wazazi damu pevu, ‘liyohishimiwa

Tukufu damu kumwagwa, pasipo ubinadamu

Ya mabavu serikali, watawala madhalimu

Wadhulumu watu wangu

Lakini, kesho, kwa jina Mungu___

Tutainuka, tupambane hadi ushindi!

Endelea kusoma shairi hili

KWA JINA LA ZANZIBAR

Kwa jinalo wewe, tungo nayandika, na kuikariri

Hitaka ujuwe, ndiwe mtukuka, ndiwe wangu huri

Sina mwenginewe, wala hatazuka, wa kumkubali

Wat’ani ni wewe, kila kitu wewe, Mama Zinjibari!

Endelea kusoma shairi hili

KIZA CHA NYOYO

Bwanatosha shukrani, mwanao kunijuliya

Tupoe sote wendani, Watani yakwangamia

Mbele ya zetu uyuni, mambo yatuharibikia

Ndilo niloshuhudia, nilipokwenda nyumbani

Endelea kusoma shairi hili


LAU WANG’OKA NINGAUNG’OWA

Natamani pumzika, hizi balaa

Yanipungue mashaka, kunilemea

Natamani kuushika, kuung’ozoa

Ungekuwa wa kung’oka, ningeung’oa!

Endelea kusoma shairi hili

HAKUNA MFANO WAKO

Hutwaa mizani, kupima utukufuwo

Hwenda chini, mno sana upandeo

Ile ya thineni, yenye tele mashindio___

Haiji chini, ni mkubwa uzitowo

Mi’ sipaoni, ushudupo mfanowo

Nife leo ama kesho, ndanimo nanichimbiwe ufuwo!

Endelea kusoma shairi hili

ULIPOPATA BUNDUKI

Ulipopata BUNDUKI:

Hukukaa msituni

Bali wekaa mjini

Kwenye raha kila fani

Soda, kuku na Pajero!

Endelea kusoma jibu hili kwa shairi la Mohammed Seif Khatib katika Fungate ya Uhuru, NIKIZIPATA BUNDUKI.

 PUNDA

Kwatakwata na mdundo, punda jasho lakutoka

Punda wenda kwa kishindo, mwendo mchaka mchaka

Mgongoniko ni rundo, bahasha la taka taka

Na bwana fimbo kashika, punda uongeze mwendo

Endelea kusoma shairi hili

YANA MWISHO

1.Haya! Kuwa ongezeka, jipe nyadhifa na vyeo

Jifanye umetukuka, kwa deko, ringo na shoo

Bali utavyotanuka, juwa una hatimayo

Yangakuwa maguuyo, mawingu hutayafika

Endelea kusoma shairi hili

CHETU CHAO, CHAO CHAO

1. Naandika kwa kilio, machozi hadi viatu

Wino ndilo kimbilio, na shahidi Mola wetu

Nayawahi haya leo, bado ningalithubutu

Naliwahi hili bao, bado lingali ni letu

Sababu hatuna chetu, vyote vishakuwa vyao

Endelea kusoma kilio hiki cha Mzanzibari katika wakati nchi yake inapochukuliwa jumla jumla na Tanganyika kwa jina la Muungano.

UHAKIKI WA KITABU CHA ‘JUMBAMARO’ I

“Kwangu mimi, nyumbani huku anakotaka kurudi Bwan’ Said hakuna tafauti kubwa na kulivyo hapa nyumbani, Zanzibar. Zanzibar ya sasa ina mambo yako shaghala baghala kama yalivyo ndotoni kwa Bwan’ Said. Maadili yanaporomoka kwa kasi kubwa mno na, ninaposoma hadithi hii ya “Msafiri”, nashindwa kuzizuia fikira zangu zisizivute picha za Kibanda Ugali (Kiwengwa), New Happy Lodge (Mji Mkongwe) au hata maeneo ya Golf, ambako kuna biashara ya tupu inayoendeshwa kwa siri ya wazi.” Endelea kusoma uhakiki huu.

UHAKIKI WA KITABU CHA ‘JUMBAMARO’ II

“Mjumbe aliyekuwepo Zanzibar alikuwa ni gazeti la Dira, ambalo lilikuwa limejitolea kuandika na kuchambua ukweli kuhusu masuala mbali mbali ya kijamii, kiuchumi na kisiasa ambayo yalihusu hatima ya Zanzibar. Lakini hilo halikuwafurahisha mabwana wa Zanzibar, na matokeo yake ni kuwa liliandamwa hadi likafungiwa moja kwa moja, huku wahusika wake wakitangazwa kuwa si raia wa nchi hii. Hapa nazungumzia Mzee wangu, Ali Nabwa, ambaye amegeuzwa mkimbizi katika nchi ya mababu na mabibi zake. Ni huzuni iliyoje kwamba hata alipokuwa anakiwekea utangulizi kitabu hiki tunachokichambua hapa, alilazimika kusaini kama TX, yaani mfanyakazi kutoka nje ya nchi. Mjumbe kaemewa” Endelea kusoma uhakiki huu.

TAMKO LA MZANZIBARI

Waliotutangulia

Nchi wakatuachia

Na wanaofuatia

Wajibu kuikutia.

Ndipo kwa huo wajibu

Tungo hii nakutubu

Iwe nayo ni sababu

Ya Watani kulindia


Endelea kusoma utenzi huu

TAFADHALI BONYEZA HAPA KUCHANGIA MAONI YAKO. UNASHAURIWA KUANDIKA MADA YA KILE UNACHOKICHANGIA.