Siasa
Mambo mengi yanafanywa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambayo yanaonyesha kutilia shaka hayo madhumuni ya kuendeleza vipaumbele vyake lakini tukio la hivi karibuni kabisa la kununua magari ya fahari kwa gharama kubwa, hili limepita kipimo. Haiwezi kuingia akilini na haikubaliki kabisa kuwa Serikali itumie fedha zilizosemwa kuwa ni za msamaha wa kodi, basi kukosekane la kufanya katika mambo yalio ya kipaumbele na zikanunuliwe magari ya kifahari. Rais Karume, Mawaziri na hata Makatibu Wakuu wote kama sisi wanaishi nchi hii na kila mmoja wetu anajua fika kuwa pamoja na ukosefu wa mfumo mzuri wa usafiri ndani ya Serikali, lakini pia suluhu si kununua magari hayo ya kifahari. Soma makala hii ya Ally Saleh.
KIKWETE NA MAPINDUZI YAKE, WAZANZIBARI NA ‘MCHEZO’ WAO

Jakaya Mrisho Kikwete, Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama: "Mtu achezee Mapinduzi aone!"
“Lakini kufika hapa nikajiuliza, hivi kwa nini Tanganyika iliipindua Zanzibar? Nikapata nadharia nyengine tatu. Moja ni woga wa Tanganyika kwamba, kuwa na jirani ambaye alikuwa anapiga hatua za kimaendeleo kwa kasi (kwa kiwango cha wakati ule) kungelikuwa na athari mbaya za kisiasa kwake, kwani wananchi wa Tanganyika wangekuja kuinuka na kudai maendeleo kama waliyokuwa wanayapata Wazanzibari kutoka kwa serikali yao. Hapa inakumbushwa kwamba hadi yanafanyika Mapinduzi, Zanzibar ilikuwa inajitegemea kiuchumi na inatoa misaada kwa nchi nyengine, ina wataalamu wa kutosha wa kizalendo na ina akiba ya kutosha kwa uwekezaji wa ndani katika hazina yake.” Soma makala hii…
ANACHOSTAHIKI MKAPA NI KURUSHIWA VIATU!

Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ni mtu wa mwisho tu kufikiri ndiye atakayeamini kuwa Mkapa alikuwa muumini wa demokrasia ya kweli na mchungaji wa haki za binaadamu. Anayetaka kuwa mkweli wa nafsi yake atafahamu kuwa mipaka ya demokrasia na haki za binaadamu kwa Mkapa ilianzia na kuishia pale nafasi ya chama chake kushika hatamu ilipohusika. Na kwa uhakika hasa, Mkapa alitumia ‘kila njia’ kuona kuwa demokrasia inafeli Zanzibar kila alipoona kuwa kupasi kwake kulimaamisha kung’olewa kwa CCM madarakani. Soma makala hii ya Salim Bimani…

Salim Bimani, Naibu Mkurugenzi wa Haki za Binaadamu na Mahusiano na Umma wa CUF
Badala yake ni Chama cha Mapinduzi (CCM) ndicho kinachoweza, kwa ushahidi kabisa kuhusishwa na kuitendea maovu Zanzibar kwa misingi ya ubaguzi, uvunjaji wa haki za binaadamu, kuvunja umoja wa kitaifa na hata kuiondolea mamlaka yake ya kujiamulia kama nchi huru. Kwa mfano, ni CCM ndiyo ambayo imekuwa ikijichorea yenyewe taswira ya chama cha kibaguzi kinachoendeshwa kwa misingi ya historia potofu ya Uarabu na Uafrika na ushahidi mmoja wa wazi ni pale, kwenye kinyang’anyiro cha tiketi ya kugombea uraisi wa Muungano mwaka 2005, kilipomkataa Salim Ahmed Salim kwa sababu tu yeye ana asili ya Kiarabu na ni Mpemba (Soma waraka wa Joseph Bukuku na kitabu cha Makwawaiya wa Kuhenga, CCM na Hatima ya Tanzania). Soma makala hii ya Salim Bimani…
MKUTANO WA WAZANZIBARI WAMALIZIKA KWA MAFANIKIO LONDON

Dkt. Yussuf Salim (kwanza kulia) mwenyekiti wa muda wa MUWAZA, katika mkutano wa London
“Kutanabahi kwamba Zanzibar inapelekwa pabaya hakujawazindua wazee tu, bali hata na hasa vijana wa siki hizi. Na ndio maana vijana hao wakachukua jukumu la kualika Wazee katika kujaribu kupanga mikakati ya kuikwamua Zanzibar hapa ilipofika. Napo kwa kweli tayari ni pahala pabaya. Kwa bahati nzuri vijana hawa hawana maruirui ya siasa za kizamani na wana muelekeo wa kutizama mbele na sio kurejearejea nyuma.” Soma mada hii ya Mwenyekiti wa muda wa MUWAZA aliyoitoa kwenye Kongamano la Wazanzibar, London, Disemba 13, 2008
BENDERA KAMA ISHARA YA UNCHI WA ZANZIBAR
“Sisi Wazanzibari hatuoni ikiwa kuna la kubishania ikiwa Zanzibar ni nchi ama la, maana ni kinyume cha mantiki kuuliza ikiwa jua linatoka mashariki ama la. Nakusudia kuwa ukweli haubishaniwi, yanayobishaniwa ni maoni ya mtu binafsi. Kwetu si suala la maoni ya mtu binafsi kwamba Zanzibar ni nchi, bali ni ukweli ulio wazi na usiopingika. Makala hii, hata hivyo, haijikiti sana huko, bali inakusudia kuonesha historia ya bendera nchini Zanzibar kwa miaka 44 iliyopita na ikiwa historia hiyo inamaanisha lolote kwa hadhi na heshima ya Zanzibar.” Soma makala hii…
TENDWA, NI CCM NDIO YA KUJIFUNZIA UCHAGUZI WA MAREKANI
“Tendwa alimsifu mgombea wa Republican, John McCain, kwa kukubali kushindwa bila ya kinyongo na kuwataka wanasiasa na Watanzania kujenga utamaduni huu wa kukubali matokeo ya uchaguzi kwa vile hali hii inasaidia kuweka mazingira mazuri ya kujipatia maendeleoa baada ya uchaguzi. Ni wito mzuri, wa hekima na busara ya hali ya juu. Lakini alichofanya Tendwa ni sawa na kutanguliza gari la farasi mbele na kutaka farasi aliyepo nyuma afanye safari ya kuelekea kule kwenye gari lake. Kama kweli Tendwa alikuwa anatoa maoni yake kutoka moyoni na kwa nia njema, basi alipaswa kuzungumzia mazingira yaliyozunguka uchaguzi wa Marekani na kulinganisha yanayoonekana Tanzania wakati wa uchaguzi.” Soma makala hii…
WAZANZIBARI HATULITAMBUI TAMKO LA SMZ
“Kwa hivyo, ikiwa tamko la SMZ linakubaliana na Rais Kikwete ambaye naye alikubaliana na Waziri Mkuu Pinda, basi sisi tunachukulia kuwa wote watatu wamekosea. Alikosea Pinda kwa kuitangaza Zanzibar si nchi akitumia Kifungu cha 1 cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano ambacho kinasema kwamba Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano bila ya kuzingatia Katiba ya Zanzibar, ambayo inaitangaza Zanzibar kuwa nchi yenye sifa zote za unchi, akakosea Kikwete kwa kumuunga mkono Pinda na sasa imekosea SMZ kwa kumuunga mkono Kikwete na kutokuheshimu Katiba yake yenyewe. Wote kwa pamoja, hoja yao inaporomoka kama mlima wa karata; na sisi tunakataa kuwa sehemu ya kuporomoka huko.” Soma makala kamili.
HAKUNA MUAFAKA KWA KUWA ZANZIBAR SI NCHI?
“Yanayotokea sasa ambayo tunaweza kuyaita ni Pinda-Gate, yaani Kashfa ya Pinda, si mambo ambayo yamezuka tu kama uyoga katika siku za umande mzuri au mimea iliyoota kwa sababu ya kupeperuka mbegu kwa upepo. Ingekuwa ni nchi za wenzetu, waandishi wangeanza kuchimba mpaka wakajua ni kwa nini Pinda akasimama kama alivyosimama, anapata nguvu wapi na nguvu zake ni za kina gani.” Endelea kusoma makala hii ya Ally Saleh
KIFICHO USIFICHE KISICHOFICHIKA
“Sitaki Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho, anishawishi niutilie shaka uelewa na uzalendo wake kwa Zanzibar, nchi ambayo yeye anasimamia moja kati mihimili mikuu ya utawala, yaani chombo cha kutunga sheria. Sitaki kabisa anilazimishe niandike jambo baya dhidi yake, kwamba ndani ya akili yake anahisabu kuwa chama chake cha Mapinduzi (CCM) kilichoko Dodoma ni kikubwa kuliko nchi yake.” Endelea kusoma makala hii.
WAZANZIBARI HAWATAKI MAFUTA YAO
Septemba 18 mwaka huu ilikuwa ya kupeana ukweli mkavu. Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar waliiambia wazi Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwamba Wazanzibari hawako tayari kuona kuwa mafuta yao yanachimbwa na kugawanywa na Tanganyika. Ulikuwa msimamo wa dhati na madhubuti. Fuatilia michango ya wajumbe hao katika semina iliyoandaliwa kwao ili wapokee taarifa ya Mshauri Muelekezi, David Reading, aliyeteuliwa na serikali mbili – ya Zanzibar na ya Muungano – eti kushauri namna bora zaidi ya ugawanaji wa gharama na mapato ya utafutaji na uchimbaji mafuta.
MUUNGANO HUU UNA AJENDA YA SIRI KWA ZANZIBAR
“Mimi si mmoja ya wale wanaoamini kwamba Muungano wa Tanganyika na Zanzibar pale mwaka 1964 ulitokana na dhamira njema walizokuwanazo wale tunaowaona kuwa waasisi wake, Sheikh Abeid Karume wa Zanzibar na Mwalimu Julius Nyerere wa Tanganyika. Sikubali kwamba msukumo wa kuungana kwa nchi hizi ulikuwa ni hisia za umoja na udugu wa Afrika (pan-africanism). Na, kwa hakika, nakerwa sana na hoja kwamba Zanzibar iliuhitaji Muungano kwa sababu ya ulinzi na kujiimarisha kiuchumi. Yote hayo yalitumiliwa tu, lakini hazikuwa sababu hasa za kuutosa utaifa wa mataifa mawili hayo.” Endelea kusoma makala hii
Kwa wale wanaodhani kwamba, kwanza, suala la kuwepo kwa Serikali ya Tanganyika ndani ya Muungano lilianzishwa na Wabunge 55 (G55) wa Tanganyika Agosti 1993 chini ya uongozi wa Njelu Kasaka, Mateo Qaresi, Arcado Ntangazwa, Mussa Nkhangaa, Jenerali Ulimwengu, Japhet Sichona, William Mlipuka, Deogratius Mwita, Sebastian Kinyondo na Tabitha Siwale; na, pili, kwamba Wazanzibari wanakurupuka sasa katika kudai haki ya nchi yao ndani ya Muungano, wanahitaji kufikiria tena na tena. Katika waraka huu ulioandikwa na kuwasilishwa nusu karne iliyopita na miaka 10 kabla ya hoja ya G55, yaani Agosti 1983, mwanasheria maarufu nchini Zanzibar, Ussi Khamis Haji, anatoa msimamo wa Wazanzibari kuhusiana na Mapendekezo ya Marekebisho ya Katiba ya Muungano na ya Zanzibar, ambayo ilisemekana yalikusudiwa kufanywa baada ya kukusanya maoni ya wananchi. Hata hivyo, ukusanyaji huo wa maoni uliishia kwa kumuondoa madarakani Rais wa Awamu ya Pili wa Zanzibar, Aboud Jumbe Mwinyi. Soma hoja kamili hapa.
SI KWELI KWAMBA SERIKALI YA TANGANYIKA HAIPO
Mawazo ya jumla waliyonayo ndugu zetu wa Tanganyika ni kwamba Wazanzibari wanafaidika zaidi na Muungano na hivyo malalamiko yao hayana msingi zaidi ya tabia mbaya ya kulialia kwa kisingizo kwamba wao ni wachache na wanatoka katika eneo dogo la Muungano huu. Lakini Juma Duni Haji anaamini kwamba ni kweli Zanzibar inakandamizwa na mfumo wa Muungano uliopo maana “viongozi wa Serikali ya Muungano hawana nia njema na Zanzibar.” Katika makala hii, ambayo ni sehemu ya waraka aliouwasilisha Aprili 26, 2007, kwenye maadhimisho ya 43 ya Muungano, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Duni anajenga hoja mpya ya uwepo wa Serikali ya Tanganyika na kuvunja ile dhana kwamba pale mwaka 1964, wakati wa Muungano, Tanganyika ilikufa. Soma makala kamili hapa.
TAFADHALI BONYEZA HAPA KUCHANGIA MAONI YAKO. UNASHAURIWA KUANDIKA MADA YA KILE UNACHOKICHANGIA.
Comments
Sorry comments are closed for this entry









i just need your help because i have opened my home-page so please i need your news through my home page.
lovely, mbarouk
well, this my home page just dealing with different things aimly to sighn zanziabrt through out the world-
lovely,
mbarouk
well, issue muhimu niniyotaka kuizungumzia kwamba jamani wazanzibar huu muungano tuangalieni sana sababu una tunyonya sisi-
cheki mfano hai kuhusu elimu ya juu-
- wizara muhimu kama za ulinzi,muungano,mambo ya ndani na masuala ya mapato-hivi tutaamka lini na kuacha sias za kipumbavu?
ikiwa leo wabunge tuna wapeleka mainland je sisi tuongozwe na nani- malaika au?
naona tusikybali kufanya majanvi sasa tuamkeni- tuacheni siasi mbovu za mmarekani an wenziwe -
ni hayo
uhuru wa kusema .com
Mimi Mzanzibari menyu.Mchango wangu kwa Wanzibari popote pale walipo wakumbuke methali hizi:- Mkataa kwao ni Mtumwa,Mcha maango hanyele hwenda akawiya papo na mama ni mama japo kuwa rikwama Rafiki yangu Ghassany anasema mama yangu Zanzibar na mimi nasema Mama yetu Zinjibari .Wito wangu nawaomba Wazanzibari tuungane kwa kushikamana pamoja kuokoa nchi yetu kwa njia ya mkato tuikatae CCM 2010
kwakweli.chakusikitisha hawa watanganyika wataendelea kutukamuampakalin nduzangu wazanzibar tuwamke tuwekitukimoja.ukiwa ccm au cuf hawowabarahawatutakiiheri sisi jaman jemnaona leo hii nchi inatutoka wazanzibar amkenwachenkasumba mtutizame1990 mpaka 2008 maishayalivokuwajuumara duufu jemnategemea kuwaatakujamwengine kutoka ccm atafanyakuwa maisharahisi tusahau niuwongo ilazikizaidi marahiitusikubatenakuwongwoza na ccm niwaongo tuu hao cuf tuwape kurazetu kwanguvumoja 2010 wazanzibar tuwepamoja kuteeya nchiyetu m