jump to navigation

Maoni

INDHARI: MAONI HAYA SI LAZIMA YAAKISI MSIMAMO WA MWENDESHAJI WA WEBLOG HII

Comments»

1. Majaliwa - October 26, 2008

“Zanzibar ilikuwa dola, taifa na nchi huru zaidi ya karne moja kabla ya Tanganyika hata kujuilikana kuwa itakuwa Tanganyika”. Kweli Zanzibar ilikua dola,lakini dola ya namna gani? Ukweli ni kwamba Zanzibar ilikua a Sultanete,yaani “Zanzibar Sultanate”.Na watu kama wewe,na babu zako,walikua watumwa chini ya sultanate hiyo,hawakua na haki kama ya watawala wao.This is a simple fact of history – nadhani yote haya unayajua na hautapinga,sasa kwanini usiseme ukweli nje nje bila kuchagua chagua vipande vya historia ya Zanzibar unavyovitaka wewe?.

2. abdalla - October 26, 2008

Ni vizuri unakomaza misuli kutetea Zanzibar lakini angalau kwa sasa ukisafiri kumbuka kuchukua bendera ya Tanzania.

3. mustafa - October 26, 2008

We mjinga sana zanzibar ilikuwa nchi wakati mkiwa watumwa wa mwarabu kama asingekuja Zanzibar usingejiona tofauti na Bara huna akili hizo Zanzibar leo hii ukiachiwa Ujitawale mtachinjana nyie maana mna chuki Zanzibar sio nchi na itaendelea kuwa sehemu ya Tanzania ama kwa viboko au bunduki ! punda haendi bila kiboko! mimi mababu zangu upande wa mama ni waasili ya Unguja na walitokea bara wakiletwa kama watumwa sasa utaniambiaje ya kuwa mi ni tofauti na watu wa bara ? we kalia historia tu historia hubadilika leo hii mtawala, kesha watwawaliwa !

4. saleem sama - October 26, 2008

kwanza nakupongeza kwa kuanzisha hii website,hongera,mimi ni Mzanzibari nnae pinga vikali siasa za CCM na CUF.Chochote tunacho zungumza Zanzibar tutizame maslahi ya wananchi sio maslahi ya watu wachache,chuki,ubinafsi na choyo ndio matatizo makubwa ya siasa za Zanzibar.Mie naunga mkono muungano wa serikali tatu,yaani serikali ya Zanzibar,serikali ya Tanganyika na serikali ya Muungano.Muungano ulikuwa muhimu kwa wakati wake lakini sasa hivi Muungano huu umepitwa na wakati haukidhi matakwa ya wakati huu,Muungano na Tanzania bara ni muhimu kwa Zanzibar kibiashara,lakini Zanzibar lazima iruhusiwe kuzungungumza na wahisani,wawekezaji wa mataifa ya nje moja kwa moja jinsi ya kuwekeza na kuisadia Zanzibar,Zanzibar haina maendeleo yeyote si elimu,ajira,afya,bara bara,kilimo,tazama uwanja wa ndege Zanzibar ni aibu,hoteli ya Bwawani inasikitisha,viwanda vyote vimekufa sukari,viatu na viwanda vidogo vidogo.Sera za CCM Zanzibar zimefeli hazifai,wananchi masikini,hawana elimu,hawana matibabu inasikitisha watu wachache tu ndo wanafaidika kwa kweli CCM imeshindwa kuleta maendeleo kwa wananchi sisi Wazanzibari kidogo sio mpaka leo hatuna maji,madaktari na hospitali,itizame TVZ imechoka.Kama kuna bahati mbaya kutokea Zanzibar ni kuundwa kwa CUF big mistake chama hiki sijui lengo lake nini?Seifu Shariff anatumia siasa za kuwagawa Wazanzibari,hofu na Upemba,inasikitisha sana image ya Seifu Shariff imeharibika ni mroho wa madaraka na hana subira,Seifu Sharif Hamad alitumiwa na Nyerere kuwaondoa madarakani Aboud Jumbe,Ramadhani Haji,Seif Bakari na Hafidh Suleiman.lakini hana subira wakakosana na Nyerere juu ya urais wa Zanzibar aliposhindana na Idris Abdul Wakil.Imani yangu mimi CCM imeshindwa kuleta maendeleo ya maisha Zanzibar,kuwaondolea wananchi kero za maisha na CUF ni chama cha Upemba kinacho wagawa Wazanzibari na kuwatia hofu na hatima isofahamika.Aboud Jumbe alikuwa mtu wa mwanzo kutoa kitabu cha kuelezea mashaka na kutoridhika na Muungano sio Seifu Shariff,kuna kila ushahidi kuwa wakati wa Nyerere Zanzibar ilikuwa inalazimishwa kuwa na Muungano na ukipinga utaondolewa madarakani kwa nguvu,Zanzibar inahitaji wasomi,madaktari,ajira,umeme,maji na kuondoa kero zote za maisha Muungano ni kiwazo cha maendeleo ya Zanzibar kwasababu unainyima Zanzibar kuongea na wahisani moja kwa moja.

5. Rajab Mohd Suleiman - October 26, 2008

nimefurahishwa sana kuona hii blog yako, sina hakika kama imeanza zamani sana, lakini kwangu mimi nimeiona leo hii kupitia blog ya michuzi,kwhivyo nakuomba uitangaze sana ili wazanzibar tuione halafu iwe ya picha kama nyengine ikiwezekana iwe ya kileo zaidi, nategemea tutakupa support ya nguvu

6. Daudi - October 27, 2008

Nyie mnaojiita wazanzibari, mtaandika mpaka sana na kulalamika hadi mwisho. Nani asiyejua kwamba wanzibari wamezoea kulalamika kusikokuwa na maana. eti mpewe madaraka ya ku-negotiate na wafadhili moja kwa moja, nani aliyewadanganya kwamba nchi inaendelea kwa misaada. Acheni uvivu wa kufikiri, dawa ni kwa viongozi kuwajibika, kuweka mikakati ya maendeleo, utalii peke yake unatosha kuwatoa, hamuhitaji cha ziada. Nyie kazi yenu kuendeleza siasa za chuki na ubaguzi. Zanzibar kuwa nchi au si nchi kunasaidia nini wewe, muhimu ni kuwa na maisha bora, afterall mataifa siku hizi yanaungana kwa manufaa yao, utaifa wao huja baadae(kwenye mechi za mpira). Shame on you, you CUF proxy

7. fauzia daudi - October 27, 2008

Asalam Aleyqum Mohammed am back again to inform you may fellow muslim kwamba tumepatwa na msiba mkubwa roho inaniuma machozi yananitoka.kumba ticket zajana za mechi baini yasimba nayanga ziliandikwa aya zamwenyezi mungu surat ikhlasi na huku tangazo lapombe yakilimanjaro.

8. Daudi - October 27, 2008

Brainless idiot! eti….. ni mwalimu msaidizi katika Idara ya Kijerumani ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA)?????? Kweli hii balaa!!!! mwalimu wa chuo kikuu hana hata digrii moja…halafu ndo mnataka kujitawala nyie. Mwalimu wa chuo kikuu!!!!!!!!! hana digrii, worse enough anafanya digrii ya kwanza kwa njia ya posta huko Tumaini.!!!???!!!! Hivi hao wanafunzi inakuwaje!!!???

HEBU wadau nisaidieni

9. Mohammed Khelef Ghassani - October 27, 2008

Leo tarehe 26 Oktoba, 2008 waliotembelea blogu hii na kuchangia ni wengi na wote nawashukuru sana. Nawashukuru wanaonipa moyo na pia nawashukuru wanaonivunja moyo. Sitajibu moja moja, bali nitachanganya, kwamba:

1. Zanzibar kuwa nchi kuna maana sana kwa hayo yanayoitwa maisha bora kwa kila mtu maana kilichoyafanya hasa maisha yawe mabaya ni kutokuwa na nguvu za kiuchumi kuusimamia uchumi wenyewe. Kwa mfano, uchumi si katika Mambo ya Muungano, lakini yale mambo yanayofanya uchumi kuwa uchumi ni ya Muungano, kama vile kodi, anga, bahari kuu, mafuta, n.k.

2. Ukweli kwamba dunia nzima sasa inaungana hausemi kwamba kuungana ni kutawaliana. Zanzibar is a less than a colony katika Muungano huu. Wazanzibari hawakatai Muungano, lakini wanataka Muungano, na Muungano tu – no more no less.

Wachangiaji walioonesha kukerwa sana na maoni haya ya Mzanzibari kwa nchi yake, wanakiri – baina ya mistari – kwamba wao ni watawala na Wazanzibari ni watawaliwa, na kwamba watalidumisha hilo vyovyote iwavyo. Vyovyote hivyo iwavyo, ndivyo hivyo vinavyivunja heshima na hadhi ya Zanzibar. Na mimi na Wazanzibari wenzangu hatuwezi kulikenulia meno hilo – hata kama pengine kwa sasa hatuwezi kulizuwia, maana hatuna nguvu za kijeshi zinazotumiwa na watawala dhidi yetu.

3. Nisiseme sana kuhusu mimi mwenyewe na uwezo wangu wa kiilimu. I am just somebody nobody and am happy with this realization, na ndio maana natafuta ilimu popote ilipo. Utamaduni wangu unanikataza kujisifu, nami sitaingia katika mtego huo kamwe!!

10. HAMAD - October 30, 2008

Assalam alaykum,
nashukuru kwa kutuwekea jukwaa hiili la kusemea sisi ambao sauti zetu hazifikii masikio ya viongozi wetu wala zikifika haziathiri nyoyo zao.
Ombi langu kwa blogger ni kutuwekea hotuba za viongozi wetu wa kitaifa, watawala na upinzani, wa Tanganyika na wa Zanzibar kwa ajili ya, si tu kusoma na kuskiliza, lakini pia kwa ajili ya marejeo pale tunapoandika au kuchangia mada katika blogi yetu hii pendwa.
Naomba kuwasilisha,
Scandinavian.

11. zanzibarsiotaifa - October 30, 2008

kumaoni yangu ingetumika hii blogi kufundishia masomo ya sayansi na hisabati ambako taifa kama letu masikini linahitaji sana na pia wapitia nafasi wa wakulima na sio wakulima jinsi ya kupata masoko ujerumani na maeneo mengine , nafasi za wanafunzi za kielimu na jinsi ya kujikomboa na umasikini nazani ingekuwa inafaa zaidi kuliko kueneza siasa za chuki ……..na ungeacha alama kubwa sana ndani ya mioyo ya WaTanzania chuki ya kidini , kikabila , nk usiombe izae sikia tuu ombaa Mungu ..uliza uambiwe utaomba ardhi ipasuke watu wanalia mpaka wanazimia wakiadithia matokeo yake ..na kwa njia hii tutafika kweli afrika mpaka wahindi watuzarau tutakuwa watumwa mpaka lini?tutatengeza mamitambo kama ya ujerumani kwa namna hii ya kubomo a inabidi tutafakari?tumia kila nafasi inayoipata kutafuta maendeleo ya kiuchumi ,kielimu na kitekinolojia kwa ajili yako na jamii yako …tusipoteze muda katika mambo yayoirudisha nyuma jamii yetu kama nyuma tuko vya kutosha kila mmoja kwa nafasi akiwajibika katika mtazamo chanya kwa nafasi yake maendeleo kwetu haya takuwa hadithi ishike uzalendo kwa watu na upendo kwao mbantu ni mbantu na sio vingine uwe muislamu hujue wewe sio muarabu uwe mkristu wewe sio mzungu kwa muhimu ni kuungana hata uko ujerumani watu wanaopewa prioriy first ni wazungu wenzao sio vingine wanajisikia kuwa wazungu na wanajivunia ardhi yao ni kwa wao sasa wewe kwa nini huwezi unasema chako ni kwa wote? tafakari kujiamini ni sehemu ya kwanza kuelekea kwenye maendeleo bila hivyo ni kapa hakuna kitu ni bila kuwa na maendeleo we ni sawa na mfu katika dunia ya sasa utanyanyasika sana kama tunanvonyasika nadhani unaona maisha yetu warusi wanasema maendeleo yako yanategemea na wewe .. hakuna mwingine wa kuendeleza Tanzania ni mimi na wewe iwe kilimanjaro ,unguja , pemba , songea, mbeya, tabora.mafia na wala sio kubomoa na ni sasa ni sio muda mwingine na bila conditions kunavitu katika maisha inabidi ukubali tu kupoteza hakuna maisha bila sadaka Mungu wabariki hawa watu na Tanzania na Afrika yao ili wawe na hekima ya maendeleo na umoja,.so bablon shall not rise again

12. zenj - November 3, 2008

sasa swali ni kama zanzibar hakuna kitu na nyinyi wabara hamnufaiki kwa jina la zanzibar kwa nini mnang”ang’ania muungano tuacheni wenyewe na uislam wetu na mafuta yetu hata kama kinibu tutajipaka

13. Rajab Mohd Suleiman - November 4, 2008

nimefurahishwa na blog hii, mimi naiita jamii ya wazanzibar ingawa watanganyika inaonekana wanaichukia kupita kiasi ushahidi ni hao maoni waliotoa hapo juu,jamani kuna ubaya gani kupigania haki yake, mtu aonewe halafu akae kimya huu sidhani kama ni ujasiri kama wenzetu wa tanganyika wanavotaka tuwe, ni naomba uendelee tu mohamedi hata kama wanakuvunja moyo, lakini nasisitiza kwamba itangaze watu wengi waijue

14. mwamba - January 28, 2009

vijana someni vizuri historia ya utumwa kwani sio waarabu pekee walohisika na biashara hii pia hao waafrika walihusika kama wanyamwezi walichukua watumwa ndani na kuleta pwani/mwambao ili wauzwe…….na utumwa uliisha mwaka 1873.sio kusema eti kabila moja tu walihusika na utumwa(soma histira) .kulikuwa na matabaka hilo si la uwongo lakini hata sasa yapo utakuta mtoto wa kizito wa serikali haguswi hata kama atafanya makosa ila mimi na wewe ndo hivyo tena.msilaumu kitu kwa chuki tu bila ya kukifatilia.pia enzi za usultani kulikuwa na haki pia kwani hao kina abudu jumbe wamesomeshwa enzi za usultani….

15. mwamba - January 28, 2009

kuhusu suala lamafuta na mdini ni kuwa haya mafuta yaliingizwa kinyemela kwa katiba ni kuwa jambo lolote la muungano linalohusu zanzibar inabidi baraza la wawakilishi liridhie jambo hilo au la jambo hilo halitokubalika kama la muungano mfano hai ni tume ya haki za binaadamu mpaka ilpokubaliwa na baraza la wawakilishi ndo ikawa inafanya kazi huko zanzibar,je hili la mafuta lini baraza lilikubali na kiridhia huu mswada ?kama halijakubali basi mafuta na mambo mengine yenye utata kuhusu zanziba ni jukumu la zanzibar hii ni kutokana na katiba,kwani hata mipaka ya baharini baina ya tanganyika na zanzibar inajulikana na hii ni kusema kmkm wakivuka mipaka hiyo serikali ya muungano ina haki ya kulalamika kwani kmkm ni ya zanzibar pekee.naona watu wanaumizana vichwa sana kuhusu kitu hichi….suluhisho ni kutizama kama hili jambo halijapitishwa na baraza la wawakilishi basi jambo hilo ni batili hii ni kwa mujibu wa katiba.kwani serikali ya muungano inaionyonya sana serikali ya muungano kwa mgawanyo huu wa 95.5 kwa 4.5….zanzibar inabidi ijikwamue yenyewe kwani hamna mtu ataesema sasa tuioneeni huruma zanzibar,ila mfumo wa muungano nao utizamwe upya kwani serikali 2 kwa nchi 2 ni kitendawili kisicho jibu,suluhu ni serikali 3 au 2 kwa maana ya kuwa muungano usikuwepo kwani haya matatizo hayatoisha kutokana na mfumo huu wa muungano.kama suala la kujiunga na OIC upande wa bara wao wanasema hii ni jumuiya ya kidini wakati kuna nchi ambazo wakaazi wake wengi ni wakristo na pia ni wanachama kama uganda,gabon,togo,suriname,kamerun nk,kama hii ni ya kiislamu je vatikan?ambao wana ubalozi hapo dar es salam ?kwa nini wao wasiondoke?tanganyika inabidi baadhi ya mambo ya zanzibar iwaachie wenyewe zanzibar kwani kuwekeana vikwazo kwenye uchumi hii ni mbaya.

16. Salim - January 31, 2009

Nachukua fursa hii kuwashukuru waanzilishi wa blog hii adhimu kwani muda mdogo tu nilioutumia basi nimejifunza mengi ambayo mengine nilikuwa sikuyajua hasa niliposoma waraka wa Mh. Juma Duni nimeweza kuchota mengi ambayo yameandikwa kitaalamu kabisa na ingefaa Wa-Zanzibari mbali mbali wakapewa kuusoma kwani ni muhimu sana kwetu kujua historia ya nchi yetu na hasa huu Muungano.

Ninachoomba tu kwa Wa-Zanzibari sote tuungane tuwe kitu kimoja kwa ajili ya kuiendeleza nchi yetu na kuilinda isimalizwe na mahasid.

Nakutakieni kila la kheri.

17. Ahmed - January 31, 2009

Asalam alaikum
Natoa shukrani zangu kwa kuanzisha blog hii, ambayo lengo lake ni kuiamsha na kuiendeleza jamii ya Kizanzibar.
Pamoja na lengo hilo zuri pia kuna udhaifu wa lunga na maneno yanayotumika katika kutoa maoni hayo. Hii imetokana na uhaba wa elimu na werevu miongoni mwa watowaji maoni. Kwa hivyo usivunjike moyo endelea na mshikamano wako huo, asaakheri ukweli uko karibu hivi.
Namalizia kwa kusema tuko nawe bega kwa bega katika kuifikia na kuiendeleza jamii ya Kizanzibar.

18. Sadiq Ali Elbaruwan - February 1, 2009

asalam aleykum,

Nimeipenda na kuifurahia sana blog yako ila naomba ndugu yangu utwekee na hotuba za viongozi wa Zanzibar wa Upinzani ili tuwasikie sauti zao na sisi tulio mbali kwani wao hawana media ilitujue sera zao na mitazamo yao kuhusu Znzibar ya leo jana na kesho, wassalaam.

19. Mohammed Khelef Ghassani - February 1, 2009

Waalykum Salaam Sheikhaan Ahmed na Sadiq,

Nashukuru kwa kutembelea weblog yetu na kwa ushauri wenu unaotia moyo. Inshallah nitaweka khutba za viongozi wa Upinzani kama mulivyoomba. Hivi sasa CUF, kwa mfano, wana weblog yao http://hakinaumma.wordpress.com, ambayo ina khutba na makala nyingi zilizoandikwa na viongozi wa juu wa chama hicho. kukhusu Chadema nadhani pia wana website yao, nadhani ni chadema.co.tz kama sikosei. Lakini nitahakikisha.

20. Haji Mbwana - February 1, 2009

Waachie hao wanaoupenda muungano wakahamie huko tanganyika watuachie zanzibar yetu.IDUMU ZANZIBAR

21. Abubakar - February 2, 2009

Babu Haji, ukweli ni kuwa hata hao wanaojifanya kuupenda Muungano kwa Zanzibar, ni wanafiki. Hawapendi Muungano wala hawaipendi Zanzibar. Wanapenda kulindiwa madaraka yao kwa kuwa wanajua kuwa Bara hufanya Mapinduzi mapya kila miaka 5.

22. hakinaumma - February 5, 2009

Maalim Seif tarehe 31 Januari alitoa hotuba nzuri kuhusu jambo hili. Pia wanawake wa mikoa mitatu ya Unguja na msoma utenzi walitoa ujumbe mzito. Sio kwamba Wazanzibari wanauchukia Muungano na wenzao wa Tanganyika, wasichokitaka wao ni nchi yao kufanywa koloni.

Hotuba, risala na utenzi vinapatikana kwenye http://hakinaumma.wordpress.com

23. abby amour - February 6, 2009

cha msingi watuachie zanzibar yetu waone kama tutashindwa kjiendeleza wenyewe sio kwani hatupati manufaa yoyote kwenye muungano kuskia mafuta yapo znz na wao wamo mbona wao wana madini tunapata pasentage ngapi.
hatuutaki muungano

24. Ahmed - February 17, 2009

Upande wetu Wazanzibar ni njia zipi tumepita kueleza matatizo yetu?
Nikiangalia ni miaka 45 tokea kuasisiwa muungano, kipi tunataka juu ya muungano huu, na hicho tunachotaka jee tumesha kidai, ikiwa tumekidai jee ni kwanjia zinazokubalika, ikiwa ombi letu halijakubaliwa jee kuna njia mbadala ya kufikisha ombi la tunachotaka juu ya muungano, ikiwa zipo ninani wa kuwasilisha ombi letu kwa njia hizo, jee rasilimali tunazo za kupeleka madai yetu?. Haya ni baadhi ya maswali ambayo binafsi huwa najiuliza, nategemea wenzangu watajiuliza zaidi ya haya. Tusifike kupanga kuwa tutajiendesha au la, kwanza tukubali nini hasa tunataka. Kama tutachukuwa watu kumi na ukauliza maoni yao juu ya muungano kila mmoja atakupa jawabu tafauti na la mwenzake. Kinachotakikana kwa Wazanzibar ni kiulekeza maoni yetu upande mmoja (converge) mfano wa tochi, tungeruhusu mwangaza utapakae pande zote basi isingekuwa na mwangazo wa kutosha, lakini kwa “converge beam of light” ndio mwangaza wake umekuwa na nguvu ya kusafiri masafa marefu.

25. Sadiq Ali Elbaruwan - February 22, 2009

asalam aleykum!
Natumai waheshimiwa nyote ni wazima na mnaendelea na harakati za maendeleo kama kawaida.
Leo mimi sitokua na maoni bali ni swali tu ambalo napenda kufahamu; mbona katika blog yetu hii hatupati habari mpya mpya kuhusiana na siasa, uchumi, na kijamii? Mimi napenda kujua hali halisi ya maendeleo ya Zanzibar, na hali kwa ujumla inaendaje! Haya Eddy endelea na kazi baba, usichoke wala usife moyo; wasomaji wako usituangushe twapenda makala kutoka blog hii!
wassalaam!

26. mwamba(mu1884@hotmail.com - February 25, 2009

a a, kwa leo napenda kutoa maoni yangu kuhusiana na khatma ya zanzibar (kwa viongozi na raia) kwani tojea 1964 mpaka hii leo manufaa ya muungano kwa zanzibar ni machache mno kwani ukipiga hatua 5 nyuma na 2 mbele kama mlevi,huwezi kusema kuwa unaendelea.kwa viongozi wa zanzibar-wingi wao hawana uzalendo kwani wakisha kuitwa na kupewa ‘ruzuku’ basi huwa teari kuisaliti nchi yao,jihadharini na dhambi hii kwani allah hatokusamehe mpaka uuombe radhi umma wa kizanzibari.tamati yangu kwa leo ni kuwa viongozi wa zanzibar (wa serikali na vyama pia ngo)wakae pamoja na kutatua matatizo ya muungano kwa majadiliano na kama tanganyika hawataki ni akheri kila mtu achukue nchi yake kwani huu ndio utakuwa mwisho wa mashaka haya.watu husema nchi kubwa huungana seuze sie! lakini hawasemi huungana vipi,kwa kuanzisha jumuiya kama eu na sio kutawalana! kuna nchi zimetengana kutokana na kuwa na muungano wa kimagube,mifano hai ni chekoslovakia,yugoslavia,urusi na ethiopia.

27. mwamba,mu1884@hotmail.com - February 25, 2009

a a,leo napenda tuangalie mfano hai wa nchi ziloungana na kutengana bila ya ushari baada ya kuona muungano hawendi,malaysia yenye ukubwa wa kilomita za mraba 329,847 na idadi ya watu kiasi cha milioni 28.malaysia iliungana na singapore tarehe 16 sept 1963na kujiengua kwenye muungano tarehe 9 aug 1965.singapore ina eneo la 707 kilomita za mraba na watu kiasi cha milioni 5.baadhi ya masharti ya muungano ni kuwa singapor iwe na baadhi ya mamlaka yake ‘autonomy’ kwenye biashara,elimu,ajira,pia haki ya utambulisho wa makabila yake…singapor ina makabila ya kichina,wamalay,na wahindi. masharti haya yalichezewa na malaysia na mwaka 1965 ikajiengua kwenye muungano kwani viongozi wao walikubali kuwa kisiwa chao ni cha mchanganyiko wa makabila na pia walikuwa thabit kutetea maslahi ya nchi/kisiwa chao.ingekuwa mpaka leo singapor imo kwenye muungano basi ingekuwa kama zanzibar,pia ukilinganisha ukubwa wa ardhi na wingi wa watu haviwiani.Tukiangalia kwetu hali ni sawa na ile ya ulokuwa muungano wa malaysia na singapor kwani hata zanzibar ina mchanganyiko mkubwa wa makabila na ina ukubwa wa kilomita za mraba 2000 na idadi ya watu kiasi cha milioni 1 wakati Tananyika ina ukubwa wa kilomita za mraba 943203 na wakaazi kiasi cha milioni 35, ukitizama yalosababisha kuvunjika muungano ule na hata hapa yapo tena ni makubwa ila sisi tumekosa viongozi thabiti na wenye mapenzi ya dhati na nchi yao kwani wao hujali maslahi yao binafsi.tuamkeni nchi inatutoka na baada ya miaka kadha tutakuja kusema YALAITI na haya ni maneno ya mjutaji.

28. bab ali - February 26, 2009

mimi na omba munijulishe kitu kimoja wapemba nao ni wanzanzibar au si wazanzibar , kwa sababu nime soma maono ya mtu moja amesema kwamba cuf ni chama cha wapemba na kinataka kuwatenganisha wazanzibar,. jawabu haraka uwezekanavyo

29. bab ali - February 26, 2009

rabi atunusuru tu laki vita vitakuwepo not too far basi jiandaeni ili tukabiliane navyo au kukimbia na tuachie nji walowezi na washezi wasio mpangilio yoyote yale lakini wakosa ni ya abed amani karume kwa kuleta muungano mwambieni huyo mtoto wa karume kuwa wabongo , hao mabwana zake walimulia babayake hao akina nyerere na wenzake ikiwa yeye haju . algun dia tiene que salir de ahi acomode lugar como quiera que sea con las buena o mala nuestra pais nos pertenese . viva PEMBA, VIVA , UNGUJA , VIVA ZANZIBAR POR FIN

30. Ahmed - March 3, 2009

Naomba kidogo ni mjibu bab ali, kitaalam kuna mambo mawili kutibu na kukinga. Ikiwa wewe ni daktari na ukakabiliwa na mgonjwa kitu cha mwanzo ni kitibu. Baadae kwa wale walio kuwa hawaja athirika kwao wao ni kukinga. Sasa kwetuy sisi tayari ni waathirika kwa hivyo tutafute njia za kutibu. Moja kati ya mambo yanayo tuathiri ni kutafuta nani mkosa. Ukianza kwa hilo itakuwa ni mlolongo wa makosa mpaka utafika karne ya nabii Musa. Kwa hivyo tutumie hekma, busara, mawazo, juhudi na sio jazba kuikomboa ZNZ. Naamini iko siku katika miaka hiyihiyi ya karibuni ZNZ itagomboka.

31. farouk - May 25, 2009

Muhammed Ass. Alykm
Nakushukuru sana kwa kazi hii nzuri nakupongeza sana na Allah atakulipa kwa kazi yako hii, jambo la pili niombi langu kwa wasomaji wote wa web log hii nikwamba tafadhali please tutumie lugha nzuri katika kuchangia japo kuwa tuna uhuru wa kusema lolote. nakutakieni kila la kheri thanks to all

32. SAID - July 23, 2009

Thanks broth. Alghassany.
Ucjali chuki binafsi just proceed.

Please remind hi ministry of ed. ya Zenj kuwa sasa zenj inahitaji tuwe na wataalamu wa mafuta na gesi kwenye nyanja tofauti. Management in gas and oil, lawyers in gas and oil,accoutant in gas and oil,policy maker in gas and oil and in different aspect. Hii bwana sio bla bla tu we have to commit and invest on it.

Kwanini serikali kazi yake inadhamini wanamusiki tu au hayo makampuni ya simu yanakubali kuwast milions of dollers on irrelevant matters. We have to respect education first starehe baadae. Kama wanataka kusaidia basi waqkati ndio huu ouil and gas hiyoo. zikija copuni kutaka kuanza kasi basi tuwe na angalau na wataalamu wa kuweza kuidhibiti hazina zetu.

ati tunataka kuanzisha sheria juu ya mafuta yasiwe ya Muungano its good ide and I amm prouding of it. But have we establish something to be seen that we are ready.

Mimi binafsi baada ya kuona this issue I made an application to one university to study Master of laws in gas and Oil. But UNFORTUNATELY Ministry of fedha and Ed hawajataka kunipatia udhamini wa masomo hayo ilhali admission bado ninayo. Lakini kwenye mambo yasio na msingi pesa huwa ipo. LA HAULA!

Au tunasubiri tuwaajiri wageni waanze kututungia sheria mbovu mbovu kwa maslahi yao.

We have to be aware that this country can only be developed by our own efforts and commitments.

Your Broth. Said.

33. Narendra Gajjar - August 17, 2009

Hiyo Gas na Mafuta inaleta Umoja ya Wazanzibari na hiyo ndo inatakiwa.
Maendeleo italetwa na wazanzibari na siyo wageni wala waheshani.
Mzee Jumbe, alisema MAPINDUZI DAIMA, mana kuendeleza na kubadlisha maisha ya Wazanzibari iwe nzuri kwa kupata Elimu,Matibabu,Malazi bora.
Sasa tujee ulize,Tulipo toka,Hapo Tulipo na Hapo Tunapo Kwenda….jee hayo MAPINDUZI DAIMA?

elly Stabby - September 7, 2009

Mawazo yenu wengi ni matatizo ni sawa na watu wanaoshabikia nyaraka za waislamu na wakristo. Zanzibar inahitaji sana muungano kwa sababu bado ina matatizo ya kiuchumi na hata haijitoleshezi kwa chakula.
Nadhani hii ni mbaya sana kung’ang’ania kuvunja muungano. Mafuta mbona hayajapatikana na watu wanauana?

Mohammed Khelef Ghassani - September 16, 2009

Elly Stabby ni kama kwamba unaishi dunia nyingine na hujui nini hasa matakwa ya Wazanzibari. Bado hatujadai kuvunja Muungano ingawa tunaweza na tunayo haki hiyo. Kwa sasa madai yetu makubwa na uwiano na uadilifu katika Muungano huu.

La kwamba Zanzibar haijitegemei kwa chakula, hilo ni kitisho kisicho maana kabisa. Kwani unadhani huo mchele wa Kyela na maharage tunayoingiza Zanzibar tunagaiwa bure na Watanganyika? Unadhani tunapunguziwa ushuru na TRA? Ni biashara. Ni kama vile ambavyo Watanganyika wanavyowauzia Wakenya na Wamalawi mahindi yao. Kwani Kenya na Malawi zimeungana na Tanganyika?

Kwani Wazanzibari wakija na pesa zao kununua mchele, hapo ambapo Muungano huu utakuwa haupo tena, Watanganyika watakaa kuwauzia? Kama wakikataa, si wataagizia Asia na Latin America kama vile wanavyoagizia magari na vitu vyengine?

Kwa hivyo, ndugu yangu Elly usitutishe nyama-rero. Tumo kwenye Muungano si kwa ajili ya kugaiwa maharage, vitunguu na nyanya. Vitu hivyo hatupewi bure, tunanunua kama vile ambavyo tunanunua Blue Band kutoka Kenya. Sawa sawa?

34. Said - October 8, 2009

Brother umesomea saikolojia mfundishe mtu afahamu na wala usimfundishe kwa hasira.

35. Harith Ghassany - October 20, 2009

Adui wa Zanzibar si Tanganyika wala si CCM. Adui wa Zanzibar ni umasikini wa ujinga tuliovikwa nao Wazanzibari na Watanganyika na Tanganyika. Siku tutakapovivuwa vizoro basi Wazanzibari na Watanganyika tutaliwacha pango la giza na kuipanda ngazi kuelekeya kunako mwangaza. Itatuchukuwa muda kabla macho kuchanganya kwa sababu giza la muda mrefu lina tabia ya kuyapofowa macho ya jamii. Chembelecho sahib na ndugu yangu mmoja, Zanzibar haitokombolewa na CUF wala na CCM bali na chama kimoja cha Uzanzibari. Soma utusomeshe brother Mohammed.