SMZ yakasirishwa na utafiti ulioonyesha Seif kinara Z`bar August 16, 2009
Posted by Mohammed Khelef Ghassani in Politics.trackback
Kampuni ya Utafiti ya Synovate Steadman imepewa wiki mbili na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) iwe imeomba radhi kwa hatua yake ya kudai kuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, ndiye anayekubalika zaidi kwa nafasi ya Urais wa Zanzibar katika uchaguzi wa 2010.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Waziri wa Nchi Afisi ya Waziri Kiongozi, Hamza Hassan Juma, alisema kampuni hiyo imefanya kitendo cha utapeli cha kuidanganya SMZ.
Alisema kampuni hiyo iliwasilisha ombi la kufanya utafiti katika barua yake ya Mei 18, mwaka huu kuhusu hali ya uchumi na utamaduni Tanzania na kupewa kibali na ofisi yake.
Alisema kampuni hiyo ambayo imesajiliwa Tanzania na kupewa namba ya usajili 32692, imefanya kinyume chake kwa kwenda kuandika mambo ya siasa na kuonyesha kuwa Hamad anaongoza kwa kukubaliwa na wananchi kwa asilimia 28 na kuwaacha wanasiasa wengine wa CCM.
Ripoti ya kampuni hiyo, ilielezwa kwamba Hamad anaongoza akifuatiwa na Dk. Mohammed Gharib Bilal mwenye alama 24, Waziri Kiongozi Shamsi Vuai Nahodha alama sita na Dk. Ali Mohammed Shein alama mbili.
“Serikali inaipa muda wa wiki mbili kuomba radhi kupitia vyombo vile vile vilivyotumika kupotosha, vinginevyo haitapewa kibali kingine chochote kufanya shughuli zake Zanzibar,”, alisema Hamza.
Kwa uapnde wa Jamhuri ya Muungano utafiti huo ulionyesha Rais Kikwete anakubalika zaidi na ana nafasi kubwa ya kutetea nafasi ya urais akifuatiwa na Mwenyekiti wa Chadema , Freeman Mbowe namba tatu ikishikwa na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba.
Hamza alisema mazingira ya Zanzibar ni tofauti na Tanzania Bara, kwa vile Zanzibar ni nchi ndogo na wananchi asilimia 60 damu zao zimejaa siasa, hivyo utafiti huo ulipaswa kuwa wa kina na kusimama kwenye mizani ya ukweli.
Alieleza kwamba uhuru wa kutoa maoni unaotolewa na serikali unapaswa utumike vizuri na sio kuwapotosha wananchi na kwamba tayari SMZ imepokea maombi mengine ya kampuni hiyo ya kutaka ifanye utafiti mwingine wa mawasiliano, lakini alisema bila ya kutekeleza agizo hilo haitapatiwa ruhusa.
CHANZO: NIPASHE
je SMZ bundi mbaya anaanza kulia sasa, hii inakuwa ni nzuri kuangalia paa akimuwinda chui.muwinda kageuka muwindwa.
we know that already haina haja ya sisi kupata utafiti,tunajua kwamba tangu mwaka alipoingia seif sharif hamad anakubalika hadi sasa tunamkubali.hiyo kampuni imetusasidia tuu kufikisha ujumbe tunashukuru sana kwa msaada wenu.
wewe mbwa vipi unaongoza mawazo ya kisenge ya wazanzibar wasenge wenzako, kumamayo zenu nyie
Ahsante Bwa’ Mkubwa kwa matusi. lakini kwa nini kama wewe ni jasiri hutumii jina lako mwenyewe, unatumia la mtu? Come open and let’s have a gentleman’s fight if you really dare.