jump to navigation

Zanzibar, Tanzania ni nchi: Kikwete kaeleweka? September 5, 2008

Posted by Mohammed Khelef Ghassani in Politics.
add a comment

Labda katika hotuba yake ya 21 Agosti 2008 Bungeni, Rais Jakaya Kikwete alikusudia kuumaliza kabisa mjadala wa ikiwa Zanzibar ni nchi au la, lakini kama ambavyo amekuwa akifeli katika mambo mengine yanayohitaji umakini na kusimamisha uongozi (providing leadership), amefeli pia katika hili. Badala yake, Rais Kikwete ameibua mjadala mzito zaidi, ukiwemo wa ikiwa kumbe Tanganyika nayo ni nchi…. Makala hii iliyochukuliwa kutoka mtandao wa ZanziNet inauhakiki mjadala huo. (more…)

Hadhi ya Zanzibar: Kwa nini JK amegonga mwamba? September 4, 2008

Posted by Mohammed Khelef Ghassani in Politics.
add a comment

Rais Jakaya Kikwete. Jibu lake kwa hadhi ya Zanzibar halijakidhi haja wala kujenga hoja. Anatakiwa aitishe mjadala wa kitaifa kuujadili Muundo wa Muungano, kwani ndio tatizo

Rais Jakaya Kikwete

Katika makala hii iliyoandikwa katika gazeti la Tanzania Daima la Septemba 3, 2008, Edward Kinabo anahoji kwamba agizo la Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwamba suala na hadhi ya Zanzibar liamuliwe na wanasheria wa pande mbili za Muungano au na vikao vya juu vya CCM halina mashiko ya kimantiki, maana tatizo hili ni la kitaifa si la kiserikali wala kichama. Badala yake anaungana na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, kudai mjadala mpana juu ya muundo mwengine wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. (more…)