Kwa la Zanzibar, CCM ya Kikwete isiwe kama ya Mkapa April 2, 2008
Posted by Mohammed Khelef Ghassani in Politics.add a comment

Licha ya kukaa madarakani kwa miaka 10 (1995-2005), Benjamin Mkapa hakutumia fursa hiyo kuutatua mgogoro wa Zanzibar badala yake aliupalilia zaidi
Na Mohammed Ghassani
Haya niyaandikayo hapa ni marejeo tu ya kile nilichokiandika karibuni mwaka mmoja nyuma, katika mwezi wa Aprili 2007. Nakirudia hapa si kuonesha tu khofu zangu kama Mzanzibari, bali pia kuonesha matarajio kama kijana mwenye matumaini ya siku za usoni kwa nchi yangu niliyoapa kuishi na kufa kwayo.
Siku chache tu kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2005, nakumbuka, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, wakati huo akiwa mgombea uraisi wa Zanzibar kwa tiketi ya chama chake, alichapisha makala katika gazeti la The East African iliyoitwa “Zanzibar fair elections is Mkapa’s legacy.”
Wakati huo tayari, kila dalili ilishaonesha kuwa uchaguzi wa Zanzibar umeshavurugwa. Tayari kulisharipotiwa kesi za kupigwa na kuteswa kwa raia wa kawaida, kuchomewa moto nyumba na mali zao, kubakwa na hata kuuliwa. Yote yalikuwa katika kipindi cha uandikishaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. (more…)
Huyu ndiye Kikwete na hii ndiyo CCM April 2, 2008
Posted by Mohammed Khelef Ghassani in Politics.1 comment so far

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Jakaya Kikwete. Ni kuelemewa, kutokuwa na nia na kukosa busara ya uongozi. Tatizo la Zanzibar ni lake na bado anajifanya si lake.
- Zanzibar iliyogawika ina maslahi zaidi kwao kuliko iliyouganika
Na Mohammed Ghassani
Hakuna la ajabu lililotokea. Nisameheni kwa kusema hivyo, lakini narudia, kilichofanywa majuzi na kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Butiama, kilikuwa kitu cha kawaida kwa chama hicho. Kuukana muafaka wa kisiasa wa Zanzibar ni kitu cha mwanzo kilichotarajiwa. Kuukubali kilikuwa kitu cha mwisho.
Kero ndio uhai wa Muungano April 2, 2008
Posted by Mohammed Khelef Ghassani in Politics.add a comment

Mohammed Seif Khatib, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Rais (Muungano). Kwa nini kila siku kero za Muungano na hazitatuki?
Na Mohammed Ghassani
Mwishoni mwa wiki iliyopita, Wazanzibari waliambiwa tena kupitia kikao cha Baraza la Wawakilishi kwamba kwenye mazungumzo baina ya ofisi ya Waziri Kiongozi wa Zanzibar na ofisi ya Waziri Mkuu wa Tanzania hakuna kikubwa kinachofanyika. Aliyelisema hilo ni mwakilishi wa jimbo la Gando, Said Ali Mbarouk, akitoa dukuduku lake kwa adha waipatayo wafanyabiashara wa Zanzibar wanaoendelea kulipishwa ushuru mara mbili na Mamlaka hiyo hiyo moja ya Mapato (TRA). (more…)