Bila ya nguvu za dola na vurugu, CCM wepesi October 30, 2007
Posted by Mohammed Khelef Ghassani in Politics.add a comment
Na Mohammed Ghassani
Naandika makala hii refu baada ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Robert Manumba, kujitokeza, wiki mbii zilizopita, kuwaasa viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mwenyekiti Freeman Mbowe na Kaimu Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe, kwamba wachunge kauli zao maana zinaweza kuwaweka pabaya kwa vile zina muelekeo wa kuvunja amani. Amani na utulivu! Misamiati ya kijanja inayotumika na Chama cha Mapinduzi (CCM) na mawakala wake kujijengea taswira kwamba wao ni watu wastaarabu, ilhali ni kinyume chake. Niweke wazi msimamo wangu kwamba naamini DCI Manumba amezungumza zaidi kisiasa kuliko ‘kiulinzi.’ (more…)