Tatizo si rushwa tu, bali ufisadi wa kisiasa September 13, 2007
Posted by Mohammed Khelef Ghassani in Politics.add a comment
Na Mohammed Ghassani
Nizungumzie kinadharia zaidi kuliko kimaada, kwani mifano hai inayohusu makala hii ya leo imekuwa mingi mno hapa Tanzania kiasi ya kwamba sisi wengine tunahisi kichefuchefu hata kuitaja. Kuna ya Richmond na Dowans, ya Karamagi na Buzwagi yake, ya ‘ujasiriamali’ wa Benjamin Mkapa na mkewe, ya Daudi Balali na minara yake pacha, ya IPTL na hiyo ya Meremeta. Uchafu tu. Uchafu mtupu unaotia kinyenyelezi cha kufumba pua na kutema mate. Po! (more…)